Friday, May 18, 2012

BALOZI WA KENYA ALIPOKUTANA NA UONGOZI NHIF

Balozi akitoa maelezo kwa ujumbe wa NHIF kuhusu utafiti aliofanya juu ya ongezeko la idadi ya watu na athari za kimazingira katika nchi za Afrika Mashariki.

Mkurugenzi Mkuu NHIF, akimpa zawadi Balozi huyo.

Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Mutinda Mutiso na Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Emanuel Humba wakisoma taarifa kuhusu tuzo ya ISSA walipokutana ofisini kwa balozi huyo.

Wakuu hao wakipeana mkono wa ahsante

NHIF na kuwaenzi wazee kwa matibabu

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umevishauri vituo vinavyotoa huduma kwa wanachama wake ambavyo vimetenga maeneo maalum, kuhakisha vinatoa huduma hiyo kwa wazee katika maeneo hayo ili kuwaepusha na usumbufu wakati wa kupata huduma za matibabu.

Rai hiyo imekuwa ikitolewa kwa nyakati tofauti na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Emanuel Humba wakati wa kutembelea hospitali, vituo vya afya na zahanati zilizosajiriwa na Mfuko huo kwa lengo la kujionea huduma zinazotolewa kwa wanachama wake.

"Lazima tuwaenzi wazee wetu, wamefanya kazi kubwa ya kuifikisha nchi hii hapa ilipo hivyo kama Mfuko tungependa kuona mahali wanapotibiwa wanachama wetu na wazee wetu nao wapate huduma mahali hapo...si vyema kuona wakitaabika wakati wa kupata matibabu," alisema Humba.

Aliwataka watoa huduma kuhakikisha wanatumia fursa mbalimbali zinazotolewa na NHIF kuboresha huduma za matibabu kwa kuwa na vifaa vya kisasa, dawa na kuboresha mazingira ya vituo hivyo.

"Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unatoa fursa ya mikopo ya vifaa tiba na ukarabati wa majengo ambao unalenga moja kwa moja kuboresha huduma za matibabu kwa wanachama wetu na wananchi kwa ujumla hivyo ni vyema wazee wetu nao wakapewa heshima kubwa wakati wa kupata matibabu," alisema Humba.

Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya ameushauri Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuongeza nguvu katika utoaji wa elimu ya afya kwa wananchi ili kupunguza gharama za matibabu.

Amesema elimu ya afya itasaidia wanachama na wananchi kwa ujumla kuepukana na maradhi ambayo yanagharimu fedha nyingi kwa ajili ya matibabu.

"Yapo maradhi yanayotokana na mtindo wa maisha kama kisukari, shinikizo la damu ambayo yanaweza kuepukika kwa wanachama wenu kupata elimu tu ya namna ya kula, kufanya mazoezi na mambo mengine," alisema Manyanya.

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, hivi karibuni umeendesha mikutano ya wadau wake katika mikoa mbalimbali nchini, ambayo kwa pamoja wameazimia kuifanya agenda ya Bima ya Afya kuwa ya kudumu.

Tuesday, April 17, 2012

Bila NHIF tungeshindwa kujiendesha-RMO

Na Grace Michael, Iringa

UONGOZI wa Hospiali ya Mkoa wa Iringa, umesema wazi kuwa bila ya kuwepo kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Hospitali hiyo ingekuwa kwenye hali ngumu ya kiundeshaji.
Kutokana na hali hiyo, uongozi wa hospitali hiyo umeahidi kutoa huduma bora kwa wanachama wa mfuko na wananchi kwa ujumla ili waone matunda ya kujiunga lakini pia wananchi wengine waweze kuona umhimu wa kujiunga na utaratibu wa Bima ya Afya.

Akizungumza baada ya kupokea msaada wa mashuka yaliyotolewa na NHIF, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Dk. Manyama, alisema kuwa msaada huo umekuja kwa wakati sahihi kutokana na uhitaji mkubwa wa mashuka unaosababishwa na idadi kubwa ya wagonjwa wanaofika hospitalini hapo.
"Tunashukuru sana wenzetu wa NHIF kwa kuliona hili, na nikiri tu kuwa bila ya uwepo wenu hata hii hospitali ingekuwa ni ngumu sana kuiendesha kwani mmekuwa mkitusaidia sana mambo mengi na fedha zenu ndizo zinatumika katika uboreshaji wa huduma za matibabu," alisema Dk. Manyama.
Alisema mahitaji ya mashuka katika hospitali hiyo ni makubwa kwa kuzingatia kwamba mashuka nane yanatakiwa kutumika kwa kila kitanda kila siku.

“Hospitali ina vitanda 365 na kwa wastani kila siku tuna wagonjwa 270 wanaolazwa huku mahitaji ya mashuka yakiwa ni nane kwa kila kitanda kwa kila siku,” alisema.

Shughuli ya kukabidhi msaada huo ilifanywa kwa nyakati tofauti jana na makamu Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Alli Kiwenge aliyekuwa ameambatana na maofisa mbalimbali wa mfuko huo.

Akiwa katika hospitali ya mkoa, Kiwenge ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (Tughe) alisema nchi inakabiliwa na changamoto kubwa ya utoaji wa huduma za afya kwa wananchi wake hasa waishio vijijini.

Alisema Idara ya Afya kwa kushirikiana na wadau wake wengine wa maendeleo wana wajibu wa kuwahamasisha wananchi hao wa vijijini kujiunga na Mfuko wa Afya wa Jamii (CHF).

“Hii ni njia ya pekee ya kumkomboa mtanzania kwa kumpa uhakika wa kutibiwa yeye na familia yake kupitia Mfuko wa Afya ya Jamii ambao upo chini ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,” alisema.

Alisema kwa kuzingatia kwamba gharama za matibabu zinapanda kila uchao na magonjwa yanaendelea kuwasibu watanzania bila kupiga hodi, mifuko hiyo ndiyo njia muafaka ya kunusuru afya zao hasa pale wanapokuwa hawana akiba ya fedha kwa ajili ya matibabu.

Alisema wanachama wa mifuko hiyo hawatakiwi kukosa matibabu au dawa na inapotokea wanakumbwa na tatizo hilo wanapaswa kutoa ripoti kwa uongozi wa NHIF ili hatua zinazohusika ikiwa ni pamoja na kufidiwa gharama za matibabu zifanyike.

Katika kituo cha Afya cha Ngome, Kiwenge aliwakumbusha wafanyakazi wa sekta ya afya kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na akasisitiza waache migomo pindi wanapotaka kudai maslahi yao.

“Fanyeni kazi, madai yenu ya mishahara na maslahi mengine tuachieni viongozi wenu, tutaendelea kuyadai kwa kukaa mezani na serikali,” alisema.

NHIF yatua Iringa, yatembelea hospitali na kutoa mashuka

Makamu wa Mwenyekiti wa NHIF, Ali Kiwenge akimkabidhi mashuka Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Manyama jana.

Mwenyekiti wa waendesha piki piki mkoa wa Iringa akitoa neno la shukrani baada ya kukabidhiwa makoti ya usalama barabarani na NHIF, kikundi hicho kimeahidi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).