Saturday, November 5, 2011

MAHAFALI YA 16 YA SEKONDARI YA AIRWING


Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dk. Makongoro Mahanga akimkabidhi zawadi mhitimu wa kidato cha nne Frola Nzosa ambayealizawadiwa kwa ajili ya nidhamu katika shule ya sekondari Airwing, Dar es Salaam jana (PICHA NA GRACE MICHAEL)

Wednesday, November 2, 2011

JAJI CHIPETA AKITOA UFAFANUZI WA TCRA

Jaji Chipeta akitoa maelezo mbele ya Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma wakati wa ukaguzi wa hesabu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), hesabu ambazo ziligonga mwamba katika kamati hiyo. (PICHA NA GRACE MICHAEL)

POAC IKIWAJIBIKA KUYABANA MASHIRIKA YA UMMA

Mjumbe wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Alphaxard Lugola wa pili kutoka kushoto akihoji jambo kwa   Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) wakati wa ukaguzi hesabu zake za mwaka jana, wengine ni wajumbe wa kamati hiyo ambayo ilikataa kupitisha hesabu za TCRA kutokana na matumizi makubwa na kutofuatwa kwa sheria ya manunuzi(PICHA NA GRACE MICHAEL)

Tuesday, November 1, 2011

UCHANGIAJI KATIKA JAMII

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dk. Makongoro Mahanga akikabidhi sh. 400,000 kama mchango wake kwa Mkurugenzi wa Shirika la Wanawake wanaoishi na Virusi vya UKIMWI mjini Morogoro.

VIJANA WAKIIGIZA

Watoto Bakari Hemed na Abubakar Saud wakiigiza kama watoto yatima katika uzinduzi wa shirika la wanawake wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Morogoro.

DK. Mahanga akiangalia kazi za mikono

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dk. Makongoro Mahanga akiangalia kazi za wajasiliamali wakati wa uzinduzi wa Shirika la Wanawake wanaoishi na Virusi vya UKIMWI mjini Morogoro mwishoni mwa mwiki.

KAMATI IKIWAJIBIKA KATIKA MAJUKUMU YAKE

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma akitoa maelekezo kwa Bodi ya NHC baada ya kupitisha hesabu zake Dar es Salaam jana.