Mradi wa Kituo cha Kisasa cha Huduma za Matibabu kinachojengwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imesema kuwa
kukamilika kwa mradi wa Kituo cha Kisasa cha Uchunguzi wa Magonjwa unaotekelezwa
na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Chuo Kikuu Dodoma utapunguza utegemezi
wa kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa kuwa kitakuwa na vifaa vya kisasa na
madaktari bingwa.
Hayo yalisemwa na Waziri wa
Kazi na Ajira Gaudensia Kabaka wakati akijibu hoja ya Kambi ya Upinzani ambayo
ilihoji faida za uwezekezaji unaofanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya katika
Chuo Kikuu cha Dodoma.
“Uwekezaji katika Chuo Kikuu
cha Dodoma
(Medicare Centre of Excellence) ni eneo mojawapo linalolenga kuhakikisha kuwa
huduma za rufaa nchini zinaimarika ikiwemo kupunguza utegemezio wa kupeleka
wagonjwa nje ya nchi,” alisema Waziri.
Alisema kuwa mradi huo
utakuwa na huduma muhimu kwa wanachama na wananchi kwa ujumla ikiwemo huduma za
matibabu ya figo, huduma za vipimo muhimu kama
Magnetic Resonance Imaging (MRI) na vipimo vingine vya uchunguzi.
Aidha kituo hicho cha kisasa
kitakuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wanaosomea shahada ya udaktari kujifunzia
kwa vitendo.
Waziri Kabaka pia litumia
fursa hiyo kufafanua kuwa, kwa mujibu wa sheria ya Mfuko huo kifungu cha 33b
kinauruhusu Mfuko kuwekeza katika vitega uchumi ambavyo vinalenga moja kwa moja
uboreshaji wa huduma za afya nchini.
|
No comments:
Post a Comment