Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Mwananzila akitia saini katika kitabu cha wageni kwenye banda la elimu la NHIF ambalo lilikuwa katika maadhimisho hayo, kushoto ni Meneja wa Kanda ya Mtwara, Joyce Sumbwe.
Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Mkoa wa Lindi, Ludovick
Mwananzila amewataka viongozi mkoani humo kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkoa ya
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuhakikisha wanaongeza kasi ya
uhamasishaji wa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili wananchi
wawe na uhakika wa kupata matibabu.
Rai hiyo aliitoa mapema wiki hii
katika maadhimisho ya siku ya siku ya Afya ya Akili Duniani. Alisema “Hakikisheni
kasi ya uhamasishaji inaongezeka na wanachi wengi wanajiunga kwenye mfuko
huu wa CHF, haiwezekani kwa mkoa wa Lindi uwe na wanachama asilimia 5.4
% tu kati ya kaya 194,424,” alisema.
Katika maadhimisho hayo, Mfuko ulishiriki
kikamilifu katika utoaji wa elimu ya namna ya kujiunga na utaratibu wa Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya na Mfuko wa Afya ya Jamii ambapo mpaka sasa mifuko hiyo
inahudumia asilimia 18.7 ya Watanzania wote.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa
alitumia fursa kuwataka viongozi mkoani humo kuhakikisha wanajipanga katika kukabiliana
na changamoto za huduma za matibabu zilizopo kwenye mkoa hususani ya uhaba
wa dawa katika vituo vya kutolea matibabu.
Kwa upande wa NHIF, akizungumzia
maadhimisho hayo, Mwakilishi wa Mkoa wa Lindi, Fortunata Kulaya alisema changamoto kubwa iko
kwenye matumizi ya fedha zinazolipwa na mfuko huo hususan za tele kwa tele
hivyo akaomba eneo hilo kuangaliwa kwa jicho la pekee ili fedha hizo ziweze
kutumika katika matumizi yaliyokusudiwa.
|
No comments:
Post a Comment