Mmoja wa wanufaika wa huduma mpya ya bima ya afya apokea kitambulisho cha matibabu kutoka kwa mgeni rasmi. |
Sunday, December 23, 2012
Mama Salma Kikwete azindua mpango maalum NHIF
Tuesday, November 13, 2012
Dk Mwinyi alivyotembelea miradi ya uwekezaji ya NHIF
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emanuel Humba akisalimiana na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii. |
Viongozi wakielekea kukagua mradi uliopo UDOM |
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF baada ya kukagua mradi. |
Ukaguzi ukiendelea |
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF akionesha namna ujenzi unavyoendelea. |
Friday, October 12, 2012
NHIF yamuenzi kipekee Mwl Nyerere
Hayati Baba wa Taifa Mwl, Julius Nyerere |
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emanuel Humba. |
KATIKA
kuhakikisha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere anaenziwa kipekee, Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya (NHIF) unaendesha zoezi la upimaji afya za wanachama na wananchi
kwa ujumla mkoani Shinyanga ambako kilele cha maadhimisho hayo yatafanyika
Oktoba 14, mwaka huu.
Akizungumzia
zoezi hilo, Mkurugenzi wa Uendeshaji Eugen Mikongoti alisema kuwa, Mfuko
umefikia uamuzi huo kwa lengo la kuenzi mazuri yote yaliyofanywa na Baba wa
Taifa enzi za uhai wake.
“Baba
wa Taifa aliapa kupigana na maadui watatu ambao ni Umasikini, Ujinga na Maradhi
na katika hayo sisi ni wadau wakubwa katika kupambana na adui maradhi na ndio
maana tumeona tumuenzi kwa njia hii ambapo wananchi watapima afya zao bila
malipo na kupata ushauri wa kitaalam ili kuepukana na maradhi yasiyoambukiza,”
alisema Mikongoti.
Mbali
na upimaji wa afya kwa wananchi, alisema kuwa Mfuko unatumia fursa hiyo kujibu
kero mbalimbali za wanachama wake ambao watafika katika viwanja vya Sabasaba ambako
Mfuko umeweka banda kwa ajili ya kuendesha zoezi la upimaji na utoaji wa elimu
juu ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Mfuko wa Afya ya Jamii, kwa muda wa
siku tano, kuanzia jana.
Alisema
kuwa lengo kubwa la NHIF ni kuhakikisha wanachama wake na wananchi kwa ujumla
wanapata huduma bora za matibabu na Vituo vya kutolea huduma hizo vinaboreshwa
kwa kuwa na vifaa vya kisasa vya uchunguzi kupitia fursa inayotolewa na Mfuko
huo ya mikopo ya vifaa tiba na ukarabati wa majengo.
“Mfuko
umekuwa na jitihada mbalimbali za kuhakikisha huduma za afya vituoni zinakuwa
bora na unafanya hivyo kwa kutambua kuwa mhimili mkubwa wa Mtanzania katika
kufanya kazi na kujiondolea umasikini ni afya yake kwanza…nawaomba wananchi wa
Shinyanga na wa maeneo mengine mfike katika banda letu ambalo linatoa huduma za
upimaji na elimu ya afya kwa ujumla,” alisema.
Mikongoti
alisema kuwa Mfuko utaendelea kumuenzi Baba wa Taifa katika kupambana na adui
maradhi kwa kuhakikisha Watanzania wanakuwa na uhakika wa matibabu kupitia
utaratibu wa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Mfuko wa Afya ya
Jamii.
Wakati
huo huo, Mfuko umeendelea na jitihada zake
za kuhakikisha makundi maalum yanapata huduma bora baada ya kuchangia jumla ya
shilingi milioni 1.5, shuka 80 na fulana 80 kwa Kituo cha Mihuji Chesire Home
kilichopo mjini Dodoma ambacho kinalea watoto wenye matatizo ya mtindio wa
ubongo.
Mchango huo wa NHIF ulitolewa
mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Dodoma katika harambee ya kuchangia kituo
hicho na Meneja wa Kanda ya Kati Dkt. Daudi Bunyinyiga ambaye alimwakilisha
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Emanuel Humba.
Akiwasilisha
mchango huo, Dokta Bunyinyiga alisema kuwa Mfuko kama Taasisi inayofanya kazi
na Jamii inawajibu wa kuhakikisha jamii inayoizunguka hususani watu wenye
mahitaji maalum wanafaidika na huduma zake.
Ongezeni kasi ya uhamasishaji CHF-RC Lindi
Maandamano ya siku ya Afya ya Akili mkoani Lindi, wa tatu kutoka kulia ni Mwakilishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Fortunatha Kulaya |
Tuesday, October 2, 2012
NHIF yasogeza huduma, yazindua ofisi mpya tisa
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza akisisitiza jambo kwa uongozi wa NHIF kwenye uzinduzi wa ofisi mpya ya Mfuko huo iliyoko Kibaha. |
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF akitoa maelezo ya awali kabla ya uzinduzi wa Ofisi hiyo. |
Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Kibaha Dk. Mpemba akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Mfuko katika uboreshaji wa huduma za matibabu. |
Baadhi ya Maofisa wa Mfuko na wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini |
Wakibadilishana mawazo namna ya uboreshaji wa huduma za matibabu mkoani Pwani |
Baadhi ya Wakurugenzi wa NHIF wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kwa hafla ya uzinduzi wa Ofisi hiyo. |
Maofisa waliokuwa wakiandaa shughuli hiyo. |
RC Mahiza aziundua ofisi mpya za NHIF
MKUU wa Mkoa wa Pwani, Bi. Mwantumu Mahiza ameutaka Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya kuisaidia kwa hali na mali Hospitali ya Tumbi kutokana
na umuhimu wake katika kuhudumia wagonjwa mbalimbali wakiwemo majeruhi wengi wa
ajali zinazotokea katika maeneo ya mkoa huo.
Alisema kuwa kutokana na changamoto nyingi zinazoikabili
Hospitali hiyo ikiwemo ya kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa kwa siku, ukosefu wa
Vifaa vya kisasa vya uchunguzi, kuna haja kubwa kwa NHIF kuingilia kati ili
kuinusuru hospitali hiyo na maisha ya Watanzania kwa ujumla.
Bi. Mahiza aliyasema hayo jana katika uzinduzi wa Ofisi
mpya ya NHIF iliyopo mkoani Pwani ambayo iliwakilisha Ofisi zingine mpya nane
zilizopo katika Mikoa ya Mara, Kigoma, Ruvuma, Rukwa, Singida, Lindi,
Shinyanga, Kagera na Manyara ambazo zimefunguliwa na NHIF kwa lengo la kusogeza
huduma kwa wanachama wake na kuboresha huduma kwa ujumla.
“Nimefarijika sana kwa kutupa heshima kubwa Mkoa wa
Pwani, mngeeamua kwenda Mkoa mwingine kuzindua ili kuziwakilisha ofisi zingine,
Niwaombe sana wenzangu NHIF, mtupe umuhimu wa kipekee katika kutusaidia vifaa
tiba na hasa kifaa cha kutunzia damu salama, inashangaza na haieleweki kwa
wasomi kama sisi kuona ajali na wagonjwa wakiwa Pwani na damu ikitunzwa Dar es
Salaam...nakuagiza Mganga Mkuu wasilisha ombi hilo NHIF haraka iwezekanavyo,”
alisema Mahiza.
Alisema kuwa suala la vifaa vya uchunguzi katika hospitali
hiyo linamnyima usingizi kutokana na mazingira yanayoikabili hospitali hiyo
ambayo kwa wastani inapokea wagonjwa 500 kwa siku.
Akijibu ombi hilo la Mkuu wa Mkoa, Mjumbe wa Bodi ya
NHIF, Bi. Mwanaidi Mtanda alisema kuwa Bodi itahakikisha inatoa kipaumbele
katika suala hilo kwa lengo la kuwezesha hospitali hiyo kuwa na vifaa vya
kisasa ili huduma bora kwa wanachama na wananchi kwa ujumla zipatikane.
“Kwa niaba ya Bodi niseme kuwa Mfuko una nia ya dhati ya
kusaidia Hospitali ya Tumbi na Mkoa wa Pwani kwa ujumla kwa lengo la kuboresha
huduma na pale tutakapopokea maombi kutoka kwenu yatafanyiwa kazi haraka sana,”
alisema Bi. Mtanda.
Bi. Mtanda hakusita kusema kuwa hamasa ya utumiaji wa
fursa inayotolewa na NHIF ya utoaji wa mikopo ya vifaa tiba na ukarabati wa
majengo kwa vituo hasa vya serikali bado ni mdogo hivyo akatumia fursa hiyo
kuwaomba viongozi na wamiliki wa vituo vyote vya matibabu vilivyosajiliwa na
Mfuko kuomba mikopo hiyo ili kuviwezesha vituo vyao kutoa huduma bora za
matibabu.
Hata hivyo, Bi. Mwantumu alieleza wazi kuwa NHIF imekuwa
chachu kubwa katika maendeleo ya sekta ya afya kutokana na ukweli kwamba vituo
vingi vinaendesha shughuli zake kwa kutumia fedha zinazolipwa na Mfuko huo.
“Mtu yeyote anayefuatilia mwenendo wa Sekta ya Afya
nchini atakubaliana nami nikisema Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, umekuwa
chachu kubwa katika maendeleo ya sekta ya afya kwani kwa kiwango kikubwa vituo
vingi vinaendesha shughuli zake kwa fedha zinazolipwa na Mfuko huo hivyo
nawapongeza na kuwataka muendelee kusaidia,” alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa NHIF, Bw. Emanuel Humba alisema
kuwa lengo la uzinduzi wa ofisi hizo ni kutaka kuwajulisha wadau kuwa Mfuko
umesogeza huduma zake karibu na wanachama ikiwa ni njia mojawapo ya uboreshaji
wa huduma.
Alisema pamoja na Mfuko huo kukua kwa kasi na kuwa na
mafanikio makubwa lakini bado unakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za
ukosefu wa dawa, vifaa tiba, upungufu wa wahudumu changamoto ambazo Mfuko
unazifanyia kazi kupitia mipango mbalimbali ikiwemo ya kusajili maduka ya dawa
muhimu na ukopeshaji wa vifaa tiba.
NHIF kwa sasa ina mtandao wa ofisi zake katika Mikoa yote
Tanzania Bara na Zanzibar isipokuwa mikoa mipya.
Wednesday, September 19, 2012
Dk. Mwinyi afanya ziara NHIF
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Emanuel Humba akiongozana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi na wajumbe wa Bodi kukagua miradi ya Mfuko huo. |
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emanuel Humba akitoa maelezo ya moja ya miradi ya Mfuko huo kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussen Mwinyi. |
Mkurugenzi wa Uwekezaji na Fedha, Deusdedit Rutazaa akitoa maelezo ya Mradi kwa Waziri na viongozi wengine wa Mfuko. |
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi akitoa maelekezo kwa viongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuhusiana na miradi iliyowekezwa Makao Makuu ya Mfuko huo. |
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Ally Kiwenge akitoa salaam za Bodi kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii. |
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii akizungumza na wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya alipofanya ziara makao makuu ya Mfuko huo leo. |
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (walioko mbele) wakisikiliza kwa makini maelekezo ya Waziri wakati akizungumza na wafanyakazi. |
Wafanyakazi wakisikiliza kwa makini maelekezo ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii. |
Subscribe to:
Posts (Atom)