Tuesday, February 21, 2012

RC: Ufanyeni Mradi wa KfW kuwa na tija

MKUU wa Mkoa Tanga Chiku Galawa amewataka viongozi mkoani humo kuhakikisha wanafanya uhamasishaji juu ya mradi wa Mama Mjamzito na Mtoto Mchanga unaofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kupitia Benki ya Ujerumani (KfW) kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bimaya Afya ili mradi huo uweze kuwa tija.

Amesema ni lazima viongozi waamke  na kuongeza mapambano ya kunusuru afya za akina mama wajawazito na watoto.

Galawa aliyasema hayo jana wakati wa uzinduzi wa Mradi huo ambao ulifanyika mkoani humo na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wafadhili wa Mradi huo, wakuu wa Wilaya, Uongozi kutoka Mkoa wa Mbeya, wanufaika wa mradi huo ambao ni akina mama wajawazito na wadau wengine.

“Uendelevu wa Mradi huu utatokana na juhudi za uelimishaji wa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii na Mfuko wa Taifa wa Bila ya Afya…natoa mwito kwa viongozi wenzangu wa Mkoa wa Tanga na Mbeya tuone fahari juu ya mradi huu muhimu na tujione wenye bahati miongoni mwa Watanzania,” alisema Galawa.

Alisema kuwa pamoja na juhudi mbalimbali ambazo zinafanywa na Serikali katika kukabiliana na changamoto za Sekta ya Afya lakini bado zimeendelea kuibuka zingine kutokana pia na kuongezeka kwa idadi watu hivyo Serikali peke yake ina mzigo mkubwa unaotakiwa kuungwa mkono na wadau wengine wa maendeleo.

“Kutokana na hali hiyo inayoikabili Serikali, daima tunaendelea kujivunia kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kuwahudumia wananchi katika maeneo tofauti ya nchi yetu kulingana na makundi yao,” alisema na kuongeza.

“Ni kazi hiyo nzuri inayofanywa na Mfuko huu ambayo imewezesha Wafadhili kutoka Serikali ya Ujerumani (KfW) kukubali kuunga mkono juhudi hizo na sasa kwa ajili ya wanawake wajawazito na watoto wachanga katika mikoa ya Tanga na Mbeya,” alisema Galawa.

Alisema mradi huo unaolenga kuboresha huduma za afya hasa kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga utasaidia akina mama kujifungua katika mazingira ya uangalizi zaidi na kuepukana na madhara ambayo wangeweza kuyapata kutokana na kujifungulia majumbani.

Galawa pia alieleza kuwa moja ya faida za mradi huo ni pamoja na kutoa vifaa tiba kama vile vitanda vya kujifungulia na vingine hivyo hatua hiyo itasaidia kutokana na ukweli kwamba vituo vingi vinakabiliwa na upungufu wa vifaa tiba.

“Ni matumaini yangu kuwa watoa huduma wa mikoa hii mtazingatia matumizi bora ya vifaa hivyo ili view endelevu na hasa kwa malengo yaliyokusudiwa,” alisema Galawa.

Kutokana na hali hiyo, aliwataka viongozi wa Halmashauri wakiongozwa na Madiwani watatekeleza wajibu wao wa kuhakikisha kwamba mradi huo unakuwa na tija na utambuzi wa akina mama hao unafanywa kwa uwazi bila upendeleo ili lengo la kuhakikisha uzazi salama kwa wanawake linatimia.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Emanuel Humba alisema kuwa lengo kubwa la mradi huo ni kuwawezesha akina mama wasio na uwezo kupata huduma za matibabu kupitia utaratibu wa NHIF katika kipindi chote cha ujauzito na miezi mitatu baada ya kujifungua.

Aidha mradi huo utasaidia kuzilipia kaya za akina mama hao mchango wa Mfuko wa Afya ya Jamii kwa kipindi cha mwaka mmoja, kuwajengea uwezo wa kifedha watoa huduma zitokanazo na Bima ya Afya.

Humba alisema kuwa mradi huo ulianza kutekelezwa katika Wilaya ya Korogwe, Pangani, Ileje na Rungwe kwa kuwaandikisha wajawazito na kuwapatia vitambulisho vya Bima ya Afya, usambazaji wa fomu 12,700 za kuandikisha walengwa ambapo mpaka hivi sasa jumla ya akina mama 600 wameshajitokeza na kuanza kufaidika.

Kutokana na hayo, Humba aliwaomba viiongozi wote wakiwemo wabunge kuhakikisha wanasaidia suala la uhamasishaji ili akina mama wengi zaidi na wasio na uwezo waweze kunufaika na Mradi huo.

Naye Mwakilishi wa KfW, Dk Kai Gesing alisema kuwa suala la afya ni suala nyeti sana hasa katika kuwasaidia akina mama wajawazito na watoto hivyo kwa kulitambua hilo, wakaona umuhimu wa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya katika kutekeleza Mradi huo.

"Suala la akina mama ni suala nyeti sana na ndio maana tumeamua kuja na Mradi huu ili hatimaye tupunguze idadi ya vifo vya akina mama hawa lakini pia kuhakikisha wengi wanajifungulia katika vituo vya afya na kwenye mazingira mazuri," alisema Dk Gesing.

Kwa upande wa wanufaika wa mradi huo ambao ni akina mama wajawazito, waliupongeza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya pamoja na wafadhili wa mradi huo kwa kuleta mradi huo ambao wao wanauona ni mkombozi wa afya zao pamoja na familia zao ambazo zitanufaika kwa matibabu kupitia CHF.

NHIF yazindua Mradi wa akina mama wajawazito na watoto wachanga Tanga

Wakiwa katika picha ya pamoja, akina mama wanne waliwawakilisha zaidi ya wanufaika 600 ambao tayari wameanza kutumia kadi za NHIF katika matibabu yao.

Wadau wa Mradi huo wakifuatilia maelezo ya mradi huo wakati wa uzinduzi.
Akikabidhi kadi kwa akina mama wanaonufaika na mradi huo.

Mkuu wa Mkoa akiangalia vitambulisho vilivyotolewa na NHIF akiwa na viongozi wa Mkoa wa Tanga na Mbeya ambako Mradi huu unatekelezwa pamoja na wafadhili wa mradi huo.

Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Bi. Zipora akipokea vitambulisho vya akina mama wajawazito wilayani kwake.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NHIF, Eugen Mikongoti kulia na Meneja wa Kanda ya Kaskazini Mashariki,Chris Mapunda wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa.

Akina mama wajawazito ambao tayari wameanza kunufaika na mradi huo kwa kupata matibabu kupitia Kitambulisho cha NHIF.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Galawa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi huo.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Hamis Mdee akifafanua jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Emanuel Humba kabla ya uzinduzi.

Mkurugenzi Mkuu Emanuel Humba akitoa maelezo ya Mradi kwa wadau mbalimbali wakiwemo wafadhili wa mradi huo ambao ni Benki ya Ujerumani (KfW)

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Galawa akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu, Humba, kushoto ni Mwakilishi wa KfW, Dk Kai Gesing.

Monday, February 13, 2012

Wanachama NHIF watibiwe kwa heshima-Humba

Na Mwandishi Wetu

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umesema kuwa unafanya kila linalowezekana ili kuhakikisha unakabiliana na changamoto zilizopo hasa za huduma kwa wanachama wake ili hatimaye waweze kupata huduma kwa heshima inayostahili.

Umesema kuwa wanachama wa Mfuko huo wanastahili kupata huduma kwa heshima kwa kuwa huduma hiyo wameilipia.

Akizungumza na watumishi wa Mfuko huo Dar es Salaam juzi wakati wa sherehe ya kukaribisha mwaka 2012, Mkurugenzi Mkuu, Emanuel Humba alisema kuwa pamoja na mafanikio makubwa ya kitaifa na kimataifa lakini bado kuna kila sababu ya kuhakikisha watumishi hao wanafanya kazi bila kuchoka kwa ajili ya wanachama na Watanzania kwa ujumla.

"Ni wazi kuwa ukiangalia tulikotoka ni kugumu zaidi, tumevuka mawimbi ya kila aina na sasa Mfuko uko pazuri na umefanikiwa kuboresha mambo mbalimbali yakiwemo mafao ya wanachama, lakini mafanikio haya yasitufanye tukaridhika, tufanyeni kazi bila kuchoka huku tukiweka mbele maslahi ya Watanzania," alisema Humba.

Alisema kuwa Mfuko huo ulianza na wanachama 164,000 mwaka 2001 lakini idadi ya wanachama imekuwa ikiongezeka kwa wastani wa asilimia 14.5 kila mwaka ambapo mpaka Desemba mwaka jana Mfuko ulikuwa na wanachama 473,771 ikiwa na maana ya wanufaika 2,509,583.

Humba pia alisema kuwa Mfuko pia umejipanga katika kuhakikisha elimu inaenezwa kwa wanachama wote wa Mfuko na wananchi kwa ujumla kwa lengo la kuzifahamu haki zao wakati wa kupata huduma lakini pia mambo ya kuzingatia kama wanachama.

Aidha alisema kuwa Mfuko umedhamiria kusogeza huduma kwa wanachama wake ambapo umeanzisha ofisi katika baadhi ya Mikoa na lengo kubwa ni kuwa na ofisi katika Mikoa yote.

Naye Mjumbe wa Bodi, Bw. Gratian Mukoba aliupongeza uongozi wa Mfuko huo kwa kuwa imara na kuufikisha hapo ulipo ukiwa na mafanikio makubwa.

Kutokana na hali hiyo, aliutaka kuendekea kuwa imara na kutoyumbishwa kwa namna yoyote ili wanachama wake waendelee kunufaika na huduma bora zinazotolewa mpaka sasa.

"Tunatambua uongozi wa Mfuko ni imara na ndio maana umeweza kuvuka mawimbi yote yaliyokuwepo na leo hii tunaona wanachama wakinufaika na mafao yaliyopo...yawezekana uimara huu umewezeshwa na aliyekikamata chombo hiki ambaye kwa kweli tuna kila sababu ya kumpongeza, uimara wake ndo unaowezesha hata haya mafanikio yaliyopo sasa," alisema Mukoba.


Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya akitoa nasaha kwa wafanyakazi.
 Kutokana na hayo, alitoa mwito kwa watumishi wa Mfuko huo kutanguliza maslahi ya Watanzania wakati wa kutimiza majukumu yao.

Watumishi NHIF watakiwa kuzingatia maslahi ya Mfuko


Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakifurahia.
 Na Mwandishi Wetu

WATUMISHI wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wametakiwa kufanya kazi huku wakilinda maslahi ya Mfuko huo na kuweka malengo ya muda mrefu ili uendelee kutoa huduma bora kwa wanachama wake.

Mwito huo ulitolewa Dar es Salaam juzi na Mjumbe wa Bodi Bi. Mariam Wilmore wakati akitoa nasaha zake kwa watumishi wa Mfuko huo wakati wa sherehe ya kukaribisha mwaka iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Alisema kuwa pamoja na sifa mbalimbali za kitaifa na Kimataifa zinazotolewa kwa Mfuko huo lakini ipo haja kwa wafanyakazi wote kujenga mshikamano na kujivunia ubima kwa lengo la kuuendeleza zaidi Mfuko na kuufanya uzidi kuwa imara.

Mbali na hayo, wajumbe wengine wa bodi walitumia fursa hiyo, kuupongeza uongozi wa Mfuko kwa kuufikisha hapo ulipo licha ya kwamba ulianza kwa kukabiliwa na changamoto nyingi ambazo zilihitaji viongozi imara na wavumilivu.

Kutokana na hali hiyo, wameutaka kuendekea kuwa imara na kutoyumbishwa kwa namna yoyote ili wanachama wake waendelee kunufaika na huduma bora zinazotolewa mpaka sasa.

"Yawezekana uimara huu umewezeshwa na aliyekikamata chombo hiki ambaye kwa kweli tuna kila sababu ya kumpongeza, uimara wake ndo unaowezesha hata haya mafanikio yaliyopo sasa," alisema Mjumbe wa Bodi, Gratian Mukoba.

Pamoja na kupongezwa kwa mafanikio yaliyofikiwa na Mfuko huo, mjumbe mwingine Prof. Joseph Shija hakusita kuwaelezwa watumishi wa Mfuko huo matumaini makubwa waliyonayo Watanzania katika Mfuko huo, hivyo akawataka kutobweteka na mafanikio yaliyofikiwa mpaka sasa na badala yake akawataka kuongeza bidii ya kazi kwa lengo la kuboresha zaidi.

"Siwezi nikashangaa kusikia mafanikio mengi ambayo mnayo mpaka sasa likiwemo la kupata Tuzo ya Kimataifa kutokana na ubora wa huduma zenu...najua kazi mliyoifanya katika kipindi hiki cha miaka 10 ni kubwa, msilewe sifa hizi ongezeni bidii katika kazi ili hatimaye mfikie lengo la afya bora kwa kila Mtanzania," alisema Prof. Shija.

Aidha aliwataka watumishi kufanya kazi kwa uadilifu na kuachana na utamaduni wa unung'unikaji lakini pia kuhakikisha wanajenga dhana ya kujiendeleza kitaaluma kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.

"Kamwe msiridhike na mlichonacho, ongezeni bidii na kujiendeleza ili utendaji uzidi kuwa bora zaidi na suala hili ili litekelezwe kwa ari, Mfuko unatakiwa kuwa na mpango wa kuwatunuku na kuwapa motisha watumishi bora kwa kila mwaka ili wengine waweze kuiga," alisema Prof. Shija.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Emanuel Humba, aliwataka watumishi kutojiona wanyonge katika hatua ambayo Mfuko iko nayo kwani ni kubwa ikilinganishwa na mifuko mingine iliyoanza kabla ya Mfuko huo.

"Mtakumbuka tulianza na changamoto nyingi sana lakini sasa tuko pazuri...watu walidiriki kutuita 'njiti' lakini hilo hatukulijali kwani kuzaliwa njiti haina maana hata akili huna na ndio maana mpaka sasa tunafanya vizuri," alisema Humba.

Kutokana na hayo, alisema kuwa Mfuko umejipanga kuhakikisha unatoa elimu ya kutosha kwa umma ili huduma zinazotolewa na Mfuko zielewe na wananchi wote lakini pia wanachama wa Mfuko huo waweze kupata huduma za matibabu kwa heshima inayotakiwa.

NHIF msiyumbishwe kwa namna yoyote-Wajumbe


Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bw. Mukoba
 Na Mwandishi Wetu

WAJUMBE wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wameupongeza uongozi wa Mfuko huo kwa kuwa imara na kuufikisha hapo ulipo ukiwa na mafanikio makubwa.

Kutokana na hali hiyo, wameutaka kuendekea kuwa imara na kutoyumbishwa kwa namna yoyote ili wanachama wake waendelee kunufaika na huduma bora zinazotolewa mpaka sasa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Dar es Salaam juzi wakati wa sherehe ya kukaribisha mwaka 2012, walisema kuwa "Tunatambua uongozi wa Mfuko ni imara na ndio maana umeweza kuvuka mawimbi yote yaliyokuwepo na leo hii tunaona wanachama wakinufaika na mafao yaliyopo,"

"Yawezekana uimara huu unawezeshwa na aliyekikamata chombo hiki ambaye kwa kweli tuna kila sababu ya kumpongeza, uimara wake ndo unaowezesha hata haya mafanikio yaliyopo sasa," alisema Mjumbe wa Bodi, Gratian Mukoba.

Pamoja na kupongezwa kwa mafanikio yaliyofikiwa na Mfuko huo, mjumbe mwingine Prof. Joseph Shija hakusita kuwaelezwa watumishi wa Mfuko huo matumaini makubwa waliyonayo Watanzania katika Mfuko huo, hivyo akawataka kutobweteka na mafanikio yaliyofikiwa mpaka sasa na badala yake akawataka kuongeza bidii ya kazi kwa lengo la kuboresha zaidi.

"Siwezi nikashangaa kusikia mafanikio mengi ambayo mnayo mpaka sasa likiwemo la kupata Tuzo ya Kimataifa kutokana na ubora wa huduma zenu...najua kazi mliyoifanya katika kipindi hiki cha miaka 10 ni kubwa, msilewe sifa hizi ongezeni bidii katika kazi ili hatimaye mfikie lengo la afya bora kwa kila Mtanzania," alisema Prof. Shija.

Aidha aliwataka watumishi kufanya kazi kwa uadilifu na kuachana na utamaduni wa unung'unikaji lakini pia kuhakikisha wanajenga dhana ya kujiendeleza kitaaluma kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.

"Kamwe msiridhike na mlichonacho, ongezeni bidii na kujiendeleza ili utendaji uzidi kuwa bora zaidi na suala hili ili litekelezwe kwa ari, Mfuko unatakiwa kuwa na mpango wa kuwatunuku na kuwapa motisha watumishi bora kwa kila mwaka ili wengine waweze kuiga," alisema Prof. Shija.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Emanuel Humba, aliwataka watumishi kutojiona wanyonge katika hatua ambayo Mfuko iko nayo kwani ni kubwa ikilinganishwa na mifuko mingine iliyoanza kabla ya Mfuko huo.

"Mtakumbuka tulianza na changamoto nyingi sana lakini sasa tuko pazuri...watu walidiriki kutuita 'njiti' lakini hilo hatukulijali kwani kuzaliwa njiti haina maana hata akili huna na ndio maana mpaka sasa tunafanya vizuri," alisema Humba.

Kutokana na hayo, alisema kuwa Mfuko umejipanga kuhakikisha unatoa elimu ya kutosha kwa umma ili huduma zinazotolewa na Mfuko zielewe na wananchi wote lakini pia wanachama wa Mfuko huo waweze kupata huduma za matibabu kwa heshima inayotakiwa.

NHIF toeni motisha kwa watumishi bora-Prof. Shija


Mjumbe wa Bodi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Prof. Shija
 Na Mwandishi Wetu

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umetakiwa kuanzisha mpango wa kutoa tuzo na motisha kwa watumishi bora ili kutoa changamoto kwa watumishi wengine.

Hatua hiyo itawezesha kufanya kazi kwa ushindani lakini pia kuongeza ufanisi na hatimaye Mfuko kuendelea kufanya vizuri katika utoaji wa huduma zake kwa wanachama.

Mwito huo ulitolewa Dar es Salaam juzi na Mjumbe wa Bodi ya Mfuko huo, Prof. Joseph Shija katika sherehe ya kukaribisha mwaka 2012 ya watumishi wa Mfuko huo.

Prof. Shija alisema kuwa Watanzania wana matumaini makubwa na Mfuko huo katika kuboresha na kuhakikisha afya bora kwa kila Mtanzania na uhakika kwa kupata matibabu kwa kadi unapatikana hivyo kuna kila sababu ya watumishi wake kufanya kazi kwa ushindani mkubwa ili kukabiliana na changamoto hiyo.

"Ili hili liweze kufanikiwa ni lazima watumishi mfanye kazi kwa uadilifu na si kwa mtindo wa unung'unikaji lakini pia hakikisheni mnajenga utamaduni wa kutoridhika na kiwango cha elimu mlichonacho, jiendelezeni kila mnapopata nafasi hiyo ili kuongeza zaidi ufanisi wa kazi zenu ndani ya shirika," alisema Prof. Shija.

Aidha aliwataka watumishi kutoridhika na viwango vya elimu walivyonavyo hivyo wajenge utamaduni wa kujiendeleza wakati wanapopata fursa hiyo ili kuufanya Mfuko huo kuwa na watumishi wenye ubora na wanaoweza kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.

Alisema kuwa Mfuko katika kipindi hiki cha miaka 10 tangu uanzishwe, umevuka mawimbi ya kila namna na kufanya mambo makubwa katika utoaji wa huduma zake ambayo yanazivuta hata nchi zingine kuja kujifunza jambo ambalo ni kuupongeza uongozi wa Mfuko huu.

Akizungumza katika sherehe hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Emanuel Humba alisema kuwa pamoja na mafanikio makubwa na ya kujivunia yaliyofikiwa na Mfuko huo, lakini bado kuna changamoto ikiwemo ya elimu kwa wananchi hasa katika kipindi hiki ambacho Mfuko unasimamia pia Mifuko ya Afya ya Jamii (CHF).

Humba alisema kuwa changamoto nyingine ni huduma kwa wananchama wa Mfuko ambapo malengo ya Mfuko ni kuhakikisha kila mwanachama anapata huduma za matibabu kwa heshima kubwa kwa kuwa wamelipia.

Hata hivyo, Humba hakusita kuwaomba watumishi hao kutojiona wanyonge mbele za umma kwa kuwa mambo yaliyofanywa na Mfuko mpaka sasa ni makubwa ikilinganishwa na namna ulivyoanza ambapo baadhi ya watu walikuwa wakiwakatisha tamaa watumishi wa mfuko huo.

"Mtakumbuka tulianza na changamoto nyingi sana lakini sasa tuko pazuri...watu walidiriki kutuita 'njiti' lakini hilo hatukulijali kwani kuzaliwa njiti haina maana hata akili huna na ndio maana mpaka sasa tunafanya vizuri hivyo hakuna sababu ya kujisikia wanyonge," alisema Humba.