KILA mpenda nchi ya Tanzania angefurahi kuona nchi hii ikibaki kisima cha utulivu na amani, wakati wa maadhimishi ya miaka 50 ya uhuru, zana mbalimbali za kivita zilioneshwa na Jeshi la Wananchi (JWTZ).
Zana hizo ni vyema zikabaki kuoneshwa kwenye maadhimisho kama haya na si kuziona zikiwa tayari kwa kufanya kazi au kwa lolote.
Binafsi nilipoziona nilitamani kuwaomba Watanzania kuilinda amani tuliyonayo kwa gharama yoyote ili siku moja tufikie ndoto ya maisha bora kwa kila Mtanzania.
Mwito wangu kwa viongozi walioko madarakani ni kuhakikisha mnaepukana na rushwa, ufisadi na mambo mengine ambayo yanawakera wananchi na kuwafanya watamani kuingia hata kwenye migogoro.
Tungependa kuona viongozi sasa mkifanya kazi zenu kwa kuzingatia maadili ya kazi zenu na kwa maslahi ya Taifa letu.
Mungu ibari Tanzania.
No comments:
Post a Comment