Na Grace Michael
SIKU moja baada ya Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Fred Mpendazoe kuanika wazi kuwa, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa
CCM, Bw. Nape Nnauye alikuwa ndio injini ya uanzishwaji wa Chama cha Jamii (CCJ) na alikuwa akivujisha siri za Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema yuko tayari kuwajibika endapo siri hizo zitatajwa hadharani.
Bw. Nnauye aliweka msimamo wake jana baada ya kuhojiwa na Majira kuhusu tuhuma mbalimbali zinazoelekezwa kwake na CHADEMA.
“Tuhuma ya mimi kuwepo kwenye mkakati wa uanzishwaji wa CCJ ni uzushi usio na mashiko kwani jana (juzi) niliposikia ndo nikaanza kuuliza hata ofisi zao zilipo...lakini kubwa waeleze pia CCJ ilikufaje na hizo siri wanazodai nilikuwa nawapa wazitaje hadharani nitawajibika,” alisema Bw. Nnauye.
Kuhusu tuhuma za kula mishahara miwili wa CCM na wa Mkuu wa Wilaya, alisema kuwa tangu ateuliwe hata mwezi haujaisha tangua ashikea nafasi hiyo hivyo kukanusha kupokea mishahara miwili.
Tuhuma nyingine ambayo ilielekezwa kwake ni ya kuhusika na kula fedha zilizotokana na ufisadi wa Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ambapo kwa hilo alidai kuwa wakati ufisadi huo ukifanyika yeye alikuwa masomoni India.
“Ushauri wangu kwa CHADEMA wajifunze kula vya kuchinja waachane na vya kunyonga,” alisema.
Akifafanua usemi huo alisema kuwa CHADEMA wanatakiwa waishi kwa kufanya kazi halali na sio kupika majungu na kupandikiza chuki kwa Watanzania kwa kuwa mwisho wa uongo ni aibu na akasema kuwa mwisho wa chama hicho umefika.
Juzi Bw. Mpendazoe akihutubia wananchi wa Mbamba Bay mkoani Ruvuma alianika mpango mzima wa waliohusika na uanzishaji wa CCJ na kuweka bayana kuwa Bw. Nnauye ndiyeo aliyekuwa akitumika kuandaa katiba ya chama hicho na kukusanya siri mbalimbali za CCM.
Alisema kuwa “Nape ni mnafiki, msaliti na mhaini ndani ya CCM kwa kuwa alishakula njama za kukiangusha CCM...tulifanya naye vikao vya siri hadi tukaanzisha CCJ leo anaitetea CCM ambayo alikuwa ameiona haifai, ni mnafiki mkubwa,” alisema Bw. Mpendazoe.
Alisema kuwa Bw. Nape ndiye alikuwa akitumika ndani ya CCJ kwenda kwa wafadhili kupokea fedha za kuanzisha chama hicho na ndiye aliyehusika kutafuta pango la chama.
Alikwenda mbali kwa kusema Rais Jakaya Kikwete anaongoza chama feki kwa kuwa kina watu wanafiki na walishamdharau kwa uongozi wake dhaifu lakini yeye aliwapa vyeo bila ya kuwajua unafiki wao.
Mpendanzoe unaonesha ni jinsi gani usivyo mtunza siri. Kama ulivyokuwa CCJ pamoja na Nape na unatoa siri zake inamaanisha ukihamia chama kingine utaendelea kutoa hata siri za CHADEMA. Naishauri CHADEMA kuwa mwangalifu sana na MPENDANZOE kwani ni mnafiki.
ReplyDeleteHata kama kweli Nape alikuwa muasissi wa ccj,hivi nyie waandishi mnashindwa kumuuliza huyo Mpendazoe wakati akianzisha ccj alikuwa hajaiona chadema. Nyie wadanganyika ni wapumbavu sana mnapakwa mafuta na wanasiasa ili mtafunwe vizuri. Mpendazoe uliishachezea hela chooni ikatumbukia
ReplyDeleteMaisha muhimu na siasa muhimu pia,ok ikiwa watu tutaamua kuwa busy na family ni sawa lakini hyo pesa tutatoa wapi?ikiwa mtaani hakuingiliki hakuna umeme hakuna huduma zozote za maana nchi inazidi kutafunwa tutakaa kimya mpk lini?
ReplyDeleteUkweli nchi haina wazalendo kabisa wapo kimaslahi zaidi,wanasiasa wote ni baba na mama m1,mimi naishi nchi moja ya middle east hii nchi haina Rais ni ya kifalme ni kweli mfalme anakula anavyotaka lakini nchi ina maendeleo ya hali ya juu wapo series kwa kila kitu nchi inafata sheria,lakini kwetu nchi ya Demokrasi haina faida yyte viongozi wizi wanakula mali za umma,Mahakama hazifanyi kazi,Taasisi za kuzuia rushwa ndio wala rushwa wakubwa tutafika lini hali hii.Viongozi wote matajiri,,,,Mungu Ibariki Tanzania huenda hata watoto watapata nafuu
Mtowa maoni ya ya mada ya uvivu sijui kaitowa wapi hiyo kauli labda angefafanua zaidi wananchi wafanye nini wakati viongozi tulionao ndio hao ambao hawana uchungu na nchi kazi yao kubwa ni kufuja mali za nchi na kujilimbikia mali wakati wanachi wao wanaishi kwa shida kubwa sana.Tanzania tuna maliasili nyingi sana kulinganisha na nchi nyingine za Afrika lakini utekelezaji wa mambo kwa viongozi wa nchi ndio tatizo kubwa sana.
ReplyDeleteBasi tufikiri kumtafuta mwanasiasa aina ya Kagame...kama kila mtu atatulia,no doubt atatokeza Lowassa,mara nyingi nimefikiri anapingwa sana kwa sababu he would have a great many greedy individuals wetting their pants!!!
ReplyDeleteMtu hazuiwi kusema chochote atakacho maana tuna uhuru wa kuongea iwe sahihi au pumba, kote ni kuongea.Hivi hao wanaoitwa wavivu wanapanga foleni kwa nani? pia ukisema watu wasisome magazeti , wewe ulijuaje kama hukusoma habari hii ktk gazeti?halafu chukua ktk hali ya kawida, wewe kama una viatu vyako kila ukivaa mara kisigino kimetoka, umekipeleka kwa fundi mara kadhaa bado hakifai, si utanunua kipya ili angalao upumzike kidogo? hali kadhalika chama kishaonekana kulegalega , achana nacho chagua wengine nao tuone utashi wao ukoje, hayo mambo ya kung'ang'ania hao hao nani anaumia? kwani nani kasema (CCM) wana HATI MILIKI YA NCHI HII? walikaa wapi kikao na MUUMBA akawambia " NINAWAUMBIA TANZANIA MTATAWALA NYIE HADI KIAMA" kila aliyeko amadrakani alikuta watu akajifunza akaweza, halafu nikuambieni inategaemea na uzalendo wa kweli wa mtu, Kagame wa Ruandwa ndiye alipanga mpango wa kutungua ndege iliyoua marais wawili mwenyewe akiwa Uganda, lakini kwa kuwa alikuwa na uzalendo,alipoingia madarakani akaondoa ukabila,maana ndo ulikuwa unasumbua, na mambo anayoyafanya sasa pale kikweli kweli yamefunika ule uasi, tofauti ya hapa Tz kule mtu kuelimisha watanzania tu kwa maneno kuhusu hali ya nchi ilivyo,hana hata mbua mkononi mwake, anaambiwa anachochea vurugu, maskini wtz, tunaridhika eti na amani na utulivu wa CCM, mdomoni tunatamka amani moyoni tunanung'unika maisha magumu, amani iliyopo tz ni mwenyezi Mungu ametufunika, na sio chama fulani msidanganyike, na kunung"unika ni dhambi bora uwe wazi ujulikane kuliko kuwa wanafiki, unafiki huzaa uasi na kuingia msituni, lakini mtu anayesema hisia zake mbele ya umma kila mtu anasikia wala hana lawama hata mbele za Mungu, kwanza nani haoni kinachoendelea TZ, kiko wazi tu na kazi tunafanya ktk mazingira hayohayo magumu, watoto wetu wanasoma ktk shule hizo hizo wanazofundishwa mambo ya computer wakati majengo yenyewe ni hoi.
ReplyDeleteBado hatujafika kwenye siasa hizo, siasa zetu hapa ni ajira tu, viongozi wetu wa kisiasa wapo pale kwa sababu wanataka waingize mapato, siasa zetu hazijabase kwenye imani bali matumbo yao na familia zao.
ReplyDeleteTanzania viongozi wanahama vyama sio kwa sababu chama hakina muelekeo anaohutaka bali ni kwa sababu kakosa cheo, tumeona hilo kwa dr.Slaa alipokatwa jina lake kugombea Ubunge kupitia CCM, leo hii utamsikia Dr.Slaa akilia kwa uchungu namna serikali inavyotoa mishahara isiyo fair lakini nyuma ya pazia yeye na mwenyekiti wake wanajitafunia tu pesa za chama chao, yeye mwenyewe anajikatia mshahara iliyo fair lakin kwenye chama chake anajikatia pande la Million 7 wakati mtumishi anayemfuatia ana Laki 6 tu,kama hauwezi kutenda fair leo utatenda ukiingia ikulu?..the beautifu one is not yet born, Mtanzania komaa na familia yako, uwe na maisha unayoyahitaji, vinginevyo kalaghabao.